Monday 27 January 2014

Mwanamke wa miaka 48 , mkazi wa Rombo akamatwa na polisi kwa kufanya ngono na watoto wa miaka 9- 14 kwa zamu


Mwanamke  mmoja aliyefahamika kwa jina la Aretas Joseph, (48), mkazi wa kijiji cha Lesoroma tarafa ya Useri, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amehojiwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wadogo wa kiume, wenye umri kati ya miaka 9 na miaka 14, jambo linaloelezwa kuwa ni shambulizi la aibu.

Akidhibitisha taarifa hiyo, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema mwanamke huyo alikamatwa Januari 8, kufuatia ushirikiano ulioonyeshwa na majirani zake baada ya kupata taarifa ya tabia yake hiyo ambayo inaelezwa amekuwa akiifanya kwa muda mrefu.

“Kufuatia taarifa walizokuwa nazo majirani hao, waliweka mtego hadi walipofanikiwa kumkuta chumbani kwake akiwa na watoto watatu wa kiume akifanya nao mapenzi,” alisema.

Kwa mujibu wa kamanda Boaz, zilikuwepo tetesi mtaani kuwa, mama huyo hufanya mapenzi na watoto wadogo, ndipo siku hiyo ya tukio majirani hao waliamua kuingia ndani kwake ili kujua ukweli wa tabia yake hiyo na kumkuta chumbani kwake akifanya mapenzi na watoto watatu.

Alisema mara baada ya majirani hao kumvizia na kumfuma mama huyo, walitoa taarifa polisi na mama huyo kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Rombo.

Kulingana na taarifa ya kamanda huyo wa Polisi, watoto hao baada ya kuojiwa walisema kuwa wapo Wanne na siku hiyo mwenzao hakuwepo na kwamba mama huyo amekuwa akiwachezea sehemu zao za siri huku akiwapaka mafuta katika sehemu zao hizo.

Aidha watoto hao walidai kuwa mara baada ya kuwachezea sehemu zao za siri, huwa anawashawishi kufanya nao mapenzi kwa zamu huku wengine wakiendelea kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake yakiwemo matiti yake.

“Watoto hao walidai kuwa, mara baada ya mama huyo kuwachezea, humtaka mmoja wao kufanya nae mapenzi na hao wengine kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake na kwenye maziwa,na baada ya kutimiza haja zake, huwataka kuondoka mara moja”alisema.

Kamanda Boaz aliendelea kusema kuwa uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha ya kuwa mwanamke huyo amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja aliekuwa amemaliza darasa la saba miaka mitano iliyopita na kujaliwa kuzaa nae mtoto mmoja.

Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa baada ya idara ya utswi wa jamii,kupata taarifa ya mahusiano hayo, idara hiyo ililifuatilia suala hilo, na hatimae kukatisha mahusiano yao hayo.

No comments: