Monday 27 January 2014

DIAMOND NA HAMISA MOBETO WADAIWA KUWA NI WAPENZI WA MUDA MREFU, WEMA SEPETU ASHAURIWA KUFUNGASHA VIRAGO


Hamisa Hassan Mobeto ambaye ni model na actress anayekimbiza katika tasnia ya filamu nchini anadaiwa kuwa mapenzini na Diamond Platinumz a.k.a Sukari ya warembo huku uhusiano wao ukidaiwa kuwa wa muda mrefu.....

Chanzo kimoja kilichodai kuwa karibu na Hamisa ambaye alishawahi kushiriki  katika  mashindano  ya  Miss Tanzania kiliuambia mtandao wa Swahiliworld  kuwa   Hamisa na Diamond  ni  wapenzi  wa  muda  mrefu  na  kwamba  Wema  Sepetu  hana  lake  kwa  Diamond:

 
 "Hivi mnajua kuwa Diamond anawachanganya kwa wakati mmoja Wema na Hamisa Mobeto?, Hamisa na Diamond ni wapenzi wa muda mrefu sana lakini  wanafanya siri...Hamisa anamwangalia tu Wema akiwewesekea penzi la Diamond huku yeye akijilia kivyake".Kilisema  chanzo  hicho

 

Hamisa alipotafutwa ili kutolea ufafanuzi madai hayo hakuweza kupatikana  mara  moja.

No comments: