Natumai
uumziwa vzur dada Violet. Me nikajana mwenye 23yrs nipo dar. Bilashaka
natumai utakua ni jibu la tatizo langu. Hapo awali nilikua na rafik ya
wakike ambae kwa dhat mimi nilikua na mpenda sana, kama unavyojua mapenz
kikohoz hakifichiki. Nilikua namuonesha dalili za waz kuwa nampenda
huku nikishindwa Kumwambia kwan yeye alionesha kuniheshimu sana. Sasa
siku 1 katka story zetu akanambia kua yeye ana mume na pia ana mtoto m1,
lkn mumewe yupo nje kimasomo. Kwa kweli hili lilinifanya nirudi nyuma
katka mchakato wangu wakutaka kumwambia ukwel kuhusu kumpenda yeye.
Lkn
ckusita nikaulizia zaid kwa shoga zake kuhusu kuolewa kwake. Kwa bahat
nzur wakanambia ukwel kuwa hajaolewa na amekudanganya tu. Sasa mimi
baada ya kuona hv nikaona anampango wa kuzuia ishara zangu za mapenz
kwake. Na hatimaye nikaona ni bora ni mueleze ukweli kuhusu moyo wangu.
Sasa siwez japo najua hajaolewa, lkn nikatumia trik hii:
nikamwambia
kuwa katka sikuzote za urafiki wetu nimekua ninajambo moyon mwangu
nataka nikueleze lkn cwez kwan we umeolewa. Akanambia hv mimi cjaolewa
nilikua nakudanganya tu, Hapo hapo ckusubir hil wala lile nikaanza
kumueleezea hali ya moyo wangu juu yake ie nampenda sana. Kwakwel yeye
hakusema chochote kwa wakati ule yaan mimi ndio nilikua naongea mwanzo
mwisho.
Sikumuacha hiv hiv bal nilivua pete yangu nakumvisha yeye jambo
ambalo lilinifanya nijihakikishe kuwa amekua wangu, baada ya hapo
tukaagana vzur tu! nakuendelea na mambo mengine. Lkn chakushangaza tena
chakushangaza tangu hapo alianza kunichukia vibaya mno, alichukia hadi
wazazi wangu wakat hapo mwanzo aliwapenda sana pindi nilivyo kua nae
kama rafik. Kwakwel dada violet ananichukia mpaka namuogopa.
Sijui nn
kimetokea, yaan salamu haitikii. Nahitaji mawazo yako dada Violet kwan
nampenda sana tena sana sanna. unadhan kwanin amekuhiv ananichukia?
No comments:
Post a Comment