Kila
mtu anajua habari za mapenzi,hata wewe unayesoma habari hii unajua
habari hizi. Mapenzi ni matunda matamu na pia ni matunda machungu.Sijui
inategemea nini lakini nadhani ni kadri unavyoyapata,unavyoyala,na
unavyojisikia wakati unaanza kula au unapomaliza.
Blog
hii ni ya watu wazima,watu wanaojua nini maana ya mapenzi au
wanaojaribu kujua zaidi.Nimeamua kuanzisha blogu hii kwa sababu najua
ipo haja ya watu kuendelea kubadilishana mawazo juu ya mapenzi,ngono na
mengineyo yanayohusiana na miili yetu,zikiwemo afya zetu.Si mnajua
kwamba kitumbua siku hizi kimeingia mchanga ndugu zangu?
Kwa
hiyo keti kitako tuanze kuyachambua masuala ya mapenzi. Kwa utaalamu
wangu wa masuala haya nadhani nitakuwa tayari kujibu maswali yenu,hoja
zenu nk kuhusiana na mapenzi,kujamiiana(ngono) na mengi mengineyo.
Jisikie huru kunitumia email au kuuliza swali lako hapa hapa,nitakujibu.
Lakini kwa kuanzisha hoja,hebu niambie,mapenzi ni nini kwa jinsi
unavyoelewa wewe?Ni kwanini eti watu
wanauana,wanafarakana,wanachinjana,nchi zinaingia kwenye vita kisa
mapenzi? Je hayo yanabakia kuwa mapenzi au chuki? Kuna uhusiano gani
kati ya mapenzi na wivu?Yupi ana nguvu kumshinda mwenzake?
No comments:
Post a Comment