Thursday 16 May 2013

ANGALIA TAARIFA MPYA KUHUSU YULE BIBI WA MIAKA 61 ...

ANGALIA TAARIFA MPYA KUHUSU YULE BIBI WA MIAKA 61 ...:
 Hii ni habari maalum kuhusu taarifa za uhakika kuhusu yule bibi wa miaka 60 aliyeua jambazi kwa risasi Bagamoyo Pwani December 9 mwaka jana. Stori za kuaminika ni kwamba bibi huyu ambae anamiliki shule mbili amekimbia nyumbani kwake na sasa hajulikani alipo, hiyo imetokana na vitisho vilivyomuandama. Siku kadhaa baada ya kufanikiwa kuua jambazi mmoja kati ya majambazi zaidi ya watano waliomvamia nyumbani kwake, Bibi alisafiri kwenda nje ya nchi kwa matibabu lakini kabla ya kurudi kwake alipata taarifa za kushtua. Uhakika wa hizo taarifa ulionyesha kwamba kundi la watu wasiojulikana wakiwa na silaha wamekua wakimuwinda. Bibi sasa hivi hapatikani kwenye simu, ameicha nyumba yake ya ghorofa ufukweni mwa bahari ya hindi na sasa anaishi kusikojulikana. Ni bibi shupavu ambae uhodari wake wa kutumia bastola kwa uzoefu wa mwaka mmoja jeshini ndio ulimfanya aue jambazi moja kati ya majambazi ambayo yalivamia nyumbani kwake December 2012, ni nyumba ya ghorofa.. na chumba cha bibi chenye sebule yake pia kiko juu lakini ngazi za kupandia ziko nje, hakuna ngazi ya ndani ndio maana ilikua rahisi majambazi kupanda walipoona mpango wa kurusha risasi wakiwa chini hauna nguvu

No comments: